array(0) { } Radio Maisha | Kamati ya bunge yamkosoa Rais kwa kutopitisha marupurupu ya wabunge wastaafu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kamati ya bunge yamkosoa Rais kwa kutopitisha marupurupu ya wabunge wastaafu

Kamati ya bunge yamkosoa Rais kwa kutopitisha marupurupu ya wabunge wastaafu

Kamati ya Bunge kuhusu Fedha imepinga maelezo ya Rais Uhuru Kenyatta kupinga kulipwa marupurupu ya shilingi laki moja kila mwezi kwa waliokuwa Wabunge hadi pale watakapofariki dunia.

Kamati hiyo chini ya uwenyekiti wa Mwakilishi wa Kike kwenye Kaunti ya Homa Bay Gladys Wanga imesema kwamba Uhuru alikosa kuliwazia suala hilo kwa kina na kuongezea kwamba waliokuwa wabunge sasa hawana uwezo wa kujikimu kimaisha kutokana na hali ngumu ya maisha.

Aidha, kamati hiyo imesema kwamba wabunge hao hupitia wakati mgumu wakati wanaposaka ajira humu nchini.

Ikumbukwe kuwa wiki mbili zilizopita, Uhuru alikataa kuidhinishwa mswada ambao ulolenga kuwalipa wabunge hao wa zamani marupurupu hayo akisema kwamba serikali haina pesa na kwamba hatua hiyo itatoa mwanya kwa wafanyakazi wengine wa umma kutaka kulipwa sawa na wabunge hao.