array(0) { } Radio Maisha | Raila awataka wauzaji wa vitabu kutoongeza bei ya vitabu shule zitakapofunguliwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila awataka wauzaji wa vitabu kutoongeza bei ya vitabu shule zitakapofunguliwa

Raila awataka wauzaji wa vitabu kutoongeza bei ya vitabu shule zitakapofunguliwa

Kinara wa ODM, Raila Odinga amewasihi wachapishaji wa vitabu kuhakikisha kwamba vitabu vyao vinauzwa kwa bei nafuu shule zikatakapofunguliwa hivi karibuni.

Raila ambaye ni mgeni wa heshima wakati wa maonesho ya vitabu ya mwaka huu - Nairobi International Bookfair ameeleza umuhimu wa wachapishahi katika kuwawezesha wanafunzi kurejelea masomo yao kwa urahisi zaidi ikizingatiwa athari za virusi vya korona kiuchumi miongoni mwa wazazi wa wanafunzi hao.

Raila ameyafungua rasmi maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa njia ya mtandao, na yatakayoendelea hadi Jumamosi huku wageni kadhaa akiwamo msomi na mwandishi Prof. Ngugi wa Thiong'o wakitarajiwa kuhutubu.