array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yasitisha mchakato wa kulivunja bunge
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mahakama yasitisha mchakato wa kulivunja bunge

Mahakama yasitisha mchakato wa kulivunja bunge

Wabunge nchini wamepata afueni baada ya mahakama kusitisha utekelezako wa agizo la Jaji Mkuu, David Maraga kutaka bunge livunjwe kwa kutopitisha Mswada wa Thuluthi Mbili ya Uwakilishi wa Kijinsia.

Jaji Weldon Korir ametoa uamuzi huo akisema Maraga hakufuata sheria katika kutoa agizo hilo. Uamuzi wake umetolewa baada ya Leina Konchella na Abdul Munasar pia kuwasilisha kesi mahakamani wakipinga agizo la Maraga.

Kupitia wakili wao Muturi Mwangi, wawili hao walimwandikia Rais Uhuru Kenyatta wakimtaka kutotii agizo hilo.

Haya yakijiri;

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Paul Kihara Kariuki amefanya mkutano na maspika Justin Muturi na Ken Lusaka kujadili hatma ya bunge baada ya Jaji Mkuu David Maraga kuagiza livunjwe kwa kutopitisha Mswada wa Thuluthi Mbili ya Uwakilishi wa Kijinsia.

Mkutano huo wa saa mbili katika majengo ya bunge pia umehudhuria na Wakili wa Serikali, Ken Ogeto. Inaarifiwa suala la kuvunjwa kwa bunge limejadiliwa kwa kina huku mikakati ya jinsi watakavyofanya kuhusu uamuzi huo ikiwekwa.

Haya yanajiri siku moja tu baada Muturi ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Huduma za Bunge, PSC akisema kwamba tume hiyo itawasilisha kesi kupinga agizo la Maraga.

Kwa mujibu wa Muturi, agizo la Maraga kutaka kufanywa kwa chaguzi ndogo katika maeneo bunge 290 na kaunti arubaini na saba chini ya siku sitini ni kinyume na sheria.

Muturi ameongeza kwamba uamuzi wa Jaji John Mativo mwaka wa 2017 kuhusu mswada huo tata, ulitolewa baada ya bunge la kumi na moja ambalo muhula wake ulikamilika miaka mitatu iliyopita kukataa kupitisha mswada wenyewe.

Muturi anasema bunge la kumi na mbili halipaswi kubebeshwa msalaba wa bunge lililopita.