array(0) { } Radio Maisha | Watu wengine 141 waambukizwa korona nchini Kenya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 141 waambukizwa korona nchini Kenya

Watu wengine 141 waambukizwa korona nchini Kenya

Kenya inaendelea katika mkondo mzuri wa kushuka kwa maambukizi ya virusi vya korona huku maambukizi yakiwa chini ya asilimia tano mara kadhaa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.

Kaimu Mkurugenzi wa Afya Daktari Partrick Amoth, amesema juhudi zilizowekwa nchini kulikabili jana la korona zimesaidia kuthibiti hali kwani kinyume na hapo awali ambapo ilibashiriwa huenda vifo kutokana na ugonjwa wa Covid 19 vingekuwa elfu tano kufikia mwishoni mwa mwaka, ilivyo sasa vifo ni 669 pekee huku maambukizi ya leo yakiwa ya asilimia 4.3.

Amoth aidha amesema badala ya kuwapima watu kwa halaiki, juhudi nyingi zimekuwa zikielekezwa katika kuwapima watu wenye hatari zaidi ya maambukizi wakiwamo wahudumu wa afya, wafungwa ambao huishi katika maeneo yenye msongamano vilevile watu wanaowasili hospitalini wakiwa na dalili zinazofanana na za korona.

Watu wengine 141 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona humu nchini baada ya kupimwa kwa sampuli elfu tatu mia tatu na saba katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Wote walioambukizwa ni Wakenya isipokuwa saba ambao ni raia wa mataifa ya kigeni. Wanaume walioambukizwa ni mia moja na watatu huku wanawake wakiwa thelathini na wanane. Mtu mchanga zaidi aliyeambukizwa ana umri wa miaka minne huku mzee zaidi akiwa na umri wa miaka sabini na minne.

Kulingana na takwimu zilizosomwa na Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya, Mercy Mwangangi, kwa mara ya kwanza Kaunti ya Trans Nzoia imeongoza kwa idadi ya maambukizi ambapo  visa ishirini na vinane vimethibitishwa kwenye kaunti hiyo.