array(0) { } Radio Maisha | Chama cha Wanasheria nchini LSK kimemwandikia Waziri wa Fedha, Ukur Yattani kusitisha mishahara ya wabunge
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Chama cha Wanasheria nchini LSK kimemwandikia Waziri wa Fedha, Ukur Yattani kusitisha mishahara ya wabunge

Chama cha Wanasheria nchini LSK kimemwandikia Waziri wa Fedha, Ukur Yattani kusitisha mishahara ya wabunge

Chama cha Wanasheria nchini LSK kimemwandikia Waziri wa Fedha, Ukur Yattani kusitisha mishahara ya wabunge na maseneta kuanzia Oktoba tarehe 12, wakati ambapo muda alio nao Rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge utakapokamilika.

Rais wa Chama hicho Nelson Havi amesema kwamba utakapofika wakati huo basi bunge halitakuwa linahudumu kisheria hivyo hakuna haja kwa wabunge kulipwa mishahara.

Aidha amesema kwamba amemwandikia Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakta Fred Matiang'i kuwapokonya walinzi wabunge hao huku akisema majengo ya bunge yanastahili kufungwa kuanzia Oktoba tarehe 12m hadi uchaguzi mwingine utakapofanyika.

Havi ameishia kwamba chama hicho kitayaandikia mashirika ya kimataifa ikiwamo Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Utoaji Mikopo IMF kuiwekea vikwazo Kenya iwapo hatua hazitachukuliwa.

Wakati uo huo, amepuuza madai ya baadhi ya wabunge kwamba iwapo bunge litavunjwa hatua hiyo itaathiri muhula wa kuhudumu wa Rais akisema matamshi kama haya yanalenga tu kuwapotosha Wakenya, huku akiwakosoa wanasiasa wanaopinga ushauri wa Jaji Mkuu, David Maraga.