array(0) { } Radio Maisha | Ann Nderitu aidhinishwa na bunge kuwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ann Nderitu aidhinishwa na bunge kuwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa

Ann Nderitu aidhinishwa na bunge kuwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa

Kamati ya Bunge la Kitaifa ya Haki na Sheria imeidhinisha uteuzi wa Anne Nderitu kuwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa. Nderitu amekuwa akishikilia wadhifa huo kikaimu tangu mwaka 2018 baada ya kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa msajili Lucy Ndung'u. Nderitu aliteuliwa na  Rais Kenyatta kwa wadhifa huo mnano Septemba 8.

Awali alikuwa akihudumu katika wadhifa wa mkuu wa usajili wa wapiga kura katika Tume ya Uchaguzi, IEBC.  Kamati hiyo ya bunge pia imeidhinisha uteuzi wa  Ali Abdulahiii na Florence Tabu kuwa wasaidizi wa msajili. 

 Hata hivyo kamati hiyo chini ya uwenyekiti wa Kigano Muturi imepinga uteuzi wa Wilson Mohochi ambaye pia aliteuliwa kuwa msaidizi wa msajili mkuu.