array(0) { } Radio Maisha | Watu watatu wanahofiwa kutekwa nyara na washukiwa wa kundi gaidi la Al Shabaab kwenye kaunti ya Mandera.
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu watatu wanahofiwa kutekwa nyara na washukiwa wa kundi gaidi la Al Shabaab kwenye kaunti ya Mandera.

Watu watatu wanahofiwa kutekwa nyara na washukiwa wa kundi gaidi la Al Shabaab kwenye kaunti ya Mandera.

Watu watatu wanahofiwa kutekwa nyara na washukiwa wa kundi gaidi la Al Shabaab kwenye kaunti ya Mandera.

Kulingana na maafisa wa polisi waliotekwa nyara ni wajenzi waliokuwa wakifanya kazi katika eneo la Lafey.

Kisa hicho kilitokea kilomita thelathini kutoka mjini Lafey wakati gari la usafiri wa umma walilokuwa wakisafiria lilivamiwa na washukiwa hao.

Inaarifiwa huenda ikawa vigumu kuwapata mateka hao kwani hawakuwa wenyeji na walikuwa katika eneo hilo kwa kazi, ambayo ingedumu muda mfupi.

Aidha inadaiwa kwamba huenda tukio hilo limechochewa na siasa za kijamii. Tukio hili limejiri wiki moja tu baada ya polisi kuwaua washukiwa watano wa kundi hilo kwenye eneo la Lafey.