×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baraza la Magavana limeonya dhidi ya kuvunjwa kwa bunge

Baraza la Magavana limeonya dhidi ya kuvunjwa kwa bunge

Baraza la Magavana limeonya dhidi ya kuvunjwa kwa bunge kufuatia agizo la Jaji Mkuu, David Maraga kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Katika taarifa, Mwenyekiti wa baraza hilo Wycliffe Oparanya amesema licha ya kwamba agizo hilo liliendana na umuhimu wa kuitekeleza katiba, itakuwa vigumu kwa bunge kuvunjwa hasa ikizingatiwa taifa linakumbwa na janga la korona.

Aidha, Oparanya amesema shughuli nyingi za serikali zitakwama iwapo Rais atatii agizo hilo. Badala yake Maraga amemtaka Rais kuwashirikisha washikadau katika sekta mbalimbali wakiwamo wataalamu wa kikatibu kufanya mashauriano ili kuepuka mkwamo wa miradi ya maendeleo nchini.

Kauli yake inajiri wakati ambapo Muungano wa Wanawake wa Mawakili, FIDA umeendeleza shutma dhidi ya wanaopinga kuvunjwa kwa bunge.

 

Tayari  Kamati ya Huduma za Bunge, PSC imetishia kuwasilisha kesi mahakamani kupinga agizo la Maraga kutaka bunge livunjwe.

 

Jumatatu wiki hii, Maraga alimwagiza Rais Kenyatta kuvunja bunge kwa kufeli kupitisha Mswada wa Thuluthi mbili wa Kijinsia.