×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto akubali shingo upande uamuzi wa Jubilee kutowania kiti cha ubunge cha Msambweni

Ruto akubali shingo upande uamuzi wa Jubilee kutowania kiti cha ubunge cha Msambweni

Naibu wa Rais William Ruto amelazimika kukubali shingo upande uamuzi wa Chama cha Jubilee wa kutokuwa na mgombea wa ubunge katika eneo la Msambweni kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge Suleiman Dori. Katibu Mkuu wa Jubilee, Raphael Tuju ametangaza kwamba ikizingatia kiti hicho kilikuwa kikishikiliwa na mwanachama wa ODM,  ni jambo la busara kutokuwa na mgombea wa Jubilee hasa baada ya ODM kuwa na ushirikiano wa utendakazi na chama hicho.

Akizungumza baada ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee Raphael Tuju pamoja na baadhi ya viongozi wa chama hicho, baada ya Tuju kutoa tangazo hilo,<AUDIO>7741

Akijibu swali iwapo uamuzi huo ulifanywa bila kuwasiliana naye, Ruto amesema kuwa kabla ya uamuzi huo Tuju alimtumia ujumbe kumweleza mapendekezo ya chama hicho lakini uamuzi ulitolewa kabla wafanye kikao rasmi.

Ikumbukwe Tuju ametangaza kuwa yeyote aliyelenga kuwania kiti cha Msambweni kupitia Chama cha Jubilee anaweza kuwania akiwa mgombea huru.

Akiulizwa iwapo atampigia debe mmoja wa wagombea wa wadhifa huo Sharlet Akinyi Onyango maarufu Sharlet Mariam ambaye alitarajia kuwania na tiketi ya Jubilee, Ruto ameelezea uwezekano wa kufanya mashauriano na mgombea yeyote atakayehitaji kuungwa mkono naye. Ikumbukwe siku chache zilizopita Sharlrt alikiasi chama cha ODM na kujiunga na Jubilee.

Tuju aidha amesema kwamba sababu nyingine ya kujiondoa katika kinyang'anyiro ni kutokana na hali ya suitafahamu kuhusu hatma ya bunge hasa baada ya Jaji Mkuu, David Maraga kupendekeza livunjwe.

Hata hivyo, kabla ya kikao hicho na Niabu wa Rais baadhi ya wafuasi na viongozi wa Jubilee walipinga uamuzi huo wa chama, Mbunge wa Soy Caleb Kositany akiwa mmoja wao. Katika ukurasa wake wa twitter Kositany alichapisha kuwa hakuna makubaliano yalifanyika kabla ya hatua hiyo. nikinukuu
"Consultation with who. There is no seat reserved for any political party. This we MUST revisit."