×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Serikali yafichua uwezekano wa kurejelewa kwa shughuli kikamilifu

Serikali yafichua uwezekano wa kurejelewa kwa shughuli kikamilifu

Wizara ya Afya imefichua uwezekano wa kurejelewa kikamilifu kwa shughuli za kiuchumi nchini kutokana na taifa kuendelea kurekodi maambukizi ya chini kwa siku za hivi karibuni.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuwa Kenya imekuwa ikirekodi maambukizi ya chini ya asilimia tano kwa majuma mawili sasa ishara kwamba huenda maambukizi yakakabiliwa kikamilifu.

Aidha ameonya kwamba hali hiyo isiwe sababu za watu kuendelea kupuuza maagizo ya serikali kwani pameshuhudiwa awamu ya pili ya maambukizi kwenye mataifa mbalimbali duniani.

Haya yanajiri huku Kenya leo hii ikithibitisha idadi ya watu mia moja thelathini ambao wameambukizwa virusi vya korona chini ya kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita baada ya kupimwa kwa sampuli 3,874 na sasa kufikisha idadi jumla ya watu walioambukizwa kuwa elfu thelathini na saba, mia tatu na arubaini na wanane.

Miongoni mwa waliombukizwa wote ni Wakenya isipokuwa saba ambao ni raia wa mataifa ya kigeni. Wanaume ni themanini na tisa huku arubaini na mmoja wakiwa wanawake. Mtu mdogo zaidi ana umri wa miaka mitatu na mkubwa miaka tisini.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi mapya huku leo watu thelathini na watano wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Aidha watu mia moja na sita wamepona Covid-19 na kufikisha idadi jumla kuwa elfu ishirini na nne mia mbili hamsini na watatu. Themanini na mmoja walikuwa  wakitibiwa hospitalini huku ishirini na watano wakiwa waliokuwa karantini nyumbani.

Hata hivyo, watu wengine watano wamefariki dunia na kufikisha idadi jumla kuwa watu mia sita sitini na sita.

Hayo yanajiri huku serikali ikihofia idadi kubwa ya watu wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani ambapo zaidi ya watu elfu 35,000 hufariki kila mwaka.

Akizungumza baada ya kuzindua kituo cha kushughulikia saratani  katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kuwa Kenya huripoti visa 5,000 vya saratani  kila mwaka.

Waziri amesema hali hiyo imechangiwa na mienendo ya maisha ya Wakenya.