array(0) { } Radio Maisha | Sudi azuiliwa kuendesha mikutano ya kisiasa hadi kesi dhidi yake itakapokamilika
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sudi azuiliwa kuendesha mikutano ya kisiasa hadi kesi dhidi yake itakapokamilika

Sudi azuiliwa kuendesha mikutano ya kisiasa hadi kesi dhidi yake itakapokamilika

Mahakama ya Nakuru imemzuia Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi kuendesha mikutano ya kisiasa hadi kesi ya uchochezi dhidi yake itakapokamilika.

Sudi amefika mahakamani mapema leo akiandamana na mawakili wake ambapo amesomewa mashtaka matatu, mawili ya uchochezi na moja la mienendo mibaya huku akiyapinga.

Hakimu wa Mahakama ya Nakuru, Lilian Arika amemzuia Sudi kuendesha mikutano yoyote ya kisiasa kati ya leo Septemba tarehe 23 na Oktoba tarehe sita wakati ambapo vikao vya kesi hiyo vitaendelea.

Awali Upande wa Mashtaka uliorodhesha mashtaka matano dhidi ya Sudi yakiwamo kutumia matamshi ya chuki, utovu wa maadili, kukataa kukamatwa, kumjeruhi afisa wa polisi na kumiliki bunduki kinyume na sheria.

Mawakili wa Sudi wakiongozwa na Isaac Terer wamefanikiwa kumwondolea Sudi mashtaka matatu likiwamo la kumjeruhi afisa wa polisi , kukataa kukamatwa na kumilika bunduki kinyume na sheria.

Mawakili hao wamesema watawasilisha ombi kupinga uamuzi wa mahakama kumzuia mteja wao kuendesha mikutano ya kisiasa.

Sudi aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia tano pesa taslimu Ijumaa iliyopita baada ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Nakuru kuendelea kumzuiliwa kwa siku saba.

Alikamatwa kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Uhuru Kenyatta na familia yake.