array(0) { } Radio Maisha | KEMSA kuuza vifaa vya kukabili korona kwa bei ya hasara
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KEMSA kuuza vifaa vya kukabili korona kwa bei ya hasara

KEMSA kuuza vifaa vya kukabili korona kwa bei ya hasara

Mamlaka ya Usambazaji wa Dawa na vifaa vya matibabu, KEMSA inalenga kutafuta mwongozo wa Baraza la Mawaziri kuuza vifaa vya kukabili maambukizi ya virusi vya korona vya shilingi bilioni 6.2 kwa bei ya hasara

Hatua hiyo ya KEMSA itasababisha hasara ya shilingi bilioni 2.3 pesa za mlipa kodi. Haya yanajiri baada ya KEMSA kuongeza mara dufu bei ya ununuzi wa vifaa hivyo na sasa hakuna ambaye anaweza kuvinunua kutokana na bei kuwa ghali.

Kwa mfano mamlaka hiyo ilinunua vifaa vywa kuwakinga madaktari dhidi ya maambukizi PPES kwa shilingi elfu tisa vifaa hivyo sasa vikiuzwa kwa shilingi elfu tatu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge Sabina Chege, amesema hali hiyo inasikitisha kwa kuwa licha ya vifaa vya KEMSA kuwa vya ubora wa hali juu, bei imeshuka humu nchini. Mamlaka hiyo imenunua vifaa vya shilingi bilioni 7.1 lakini imefanikiwa tu kuuza vifaa vya milioni moja pekee.

Tayari maafisa wake wanachungzwa wakihusishwa na wizi wa mabilioni ya fedha za ununuzi wa vifaa vya kukabili maambukizi.