array(0) { } Radio Maisha | Kinoti ataka Malala kushtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu polisi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kinoti ataka Malala kushtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu polisi

Kinoti ataka Malala kushtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu polisi

Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, DCI,  George Kinoti  amependekeza Seneta wa Kakamega, Malala kufunguliwa mashtaka ya kutoa taarifa zisizo na msingi kuhusu njama ya kumwangamiza. Akizungumza mbele ya Kamati ya Seneti ya Usalama na ile ya  Haki na Sheria,  Kinoti amesema baada ya kufanya uchunguzi wa madai yaliyoibuliwa na Malala, walibaini kwamba hayakuwa ya kweli na yaliyokuwa na njama fiche. Anesema ni kinyume cha sheria kuibua madai mazito yasiyo na msingi.

Kinoti aidha amemtaka Malala kuomba msamaha kwa kuwaharibia sifa maafisa wa usalama aliyodai walikuwa na njama ya kumwangamiza. Kinoti aidha amesema maafisa ambao madai yaliibuliwa dhidi yao wameathirika pakubwa kisaikolojia  na wanastahili kuombwa msamaha.

Aidha Kinoti amesema hoteli ya Eaton ambayo maafisa hao wanadaiwa kupanga njama ya kumwangamiza Malala haipo vilevile kusema kwamba hakuna eneo maalum katika ofisi za DCI ambalo maafisa hao vilevile wanadaiwa kupanga njama hiyo.


Wiki iliyopita Malala aliyekuwa akitiririkwa na machozi alilieleza bunge kwamba  maisha yake yalikuwa hatarini akidai kuwa kuna baadhi ya maafisa wa polisi waliotumwa kumwangamiza. Awali Malala alisema huenda njama hiyo ilichochewa na msimamo wake wa kupinga mfumo wa ugavi wa mapato ya kaunti japo baadaye mfumo huo uliidhinishwa huku Malala akiwa miongoni mwa walioudhinisha baada ya kufanyiwa marekebisho na Kamati ya Seneti ya watu 12 iliyopewa jukumu la kutafuta mwafaka.

Wakati uo huo, Inspekta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai ambaye pia amefika mbele ya kamati hiyo ya pamoja ameagiza kurejeshwa kwa walinzi wa wabunge wote ambao inadaiwa walitwaliwa kutokana na misimamo yao ya kutoiunga mkono serikali. Mutyambai ametoa agizo hilo baada ya maseneta akiwamo Kipchumba Murkomen wa Elgeyo Marakwet kumtaka kueleza sababu za kuondolewa kwa walinzi hao.