array(0) { } Radio Maisha | Jaji Mkuu David Maraga ashtumiwa kwa kutozingatia sheria katika ushauri wa kutaka bunge kuvunjwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jaji Mkuu David Maraga ashtumiwa kwa kutozingatia sheria katika ushauri wa kutaka bunge kuvunjwa

Jaji Mkuu David Maraga ashtumiwa kwa kutozingatia sheria katika ushauri wa kutaka bunge kuvunjwa

Jaji Mkuu David Maraga ameshtumiwa kwa kutozingatia utaratibu ufaao alipomkabidhi Rais Uhuru Kenyatta waraka wenye ushauri wa kulivunja bunge kwa kutoidhinisha mswada wa uwakilishi sawa wa kijinsia kwa mujibu wa katiba.

Akihojiwa wakati wa kipindi cha Maisha Asubuhi, hapa Radio Maisha, Seneta wa Makueni, Mutula Kilonzo Junior ambaye pia ni wakili, amesema kwamba alichostahili kufanya Maraga ni kuwasilisha waraka kwa bunge kulifahamisha kuhusu hatua alizolenga kuchukua kufuatia kutopitishwa kwa mswada huo ili kupata maoni ya bunge kabla ya kuchukua hatua  yoyote ile.

Mutula aidha ametoa kauli inayofanana na ya Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi kwamba waraka uliowasilishwa awali na mahakama ulitumwa kwa bunge lililotanguliwa wala si bunge la sasa.

Aidha, amesema ilivyo sasa bunge likivunjwa kisha uchaguzi mwingine ufanyike, hali hiyo huenda ikaibua mgogoro kuhusu hatamu ya uongozi ya wabunge watakaochaguliwa ikizingatiwa uchaguzi mkuu unafaa kufanyika mwaka 2022 kwa mujibu wa katiba.

Seneta huyo wa Makueni amesema suala la uwakilishi sawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi linafaa kujumuishwa katika mpango wa BBI ili mwongozo dhabiti uwekwe kuhusu namna hitaji hilo litakavyoafikiwa ili uchaguzi mwingine utakapofanyika iwe bayana namna ya kuwachagua viongozi.