×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KNUT yawataka walimu kufika shuleni kuanzia Jumatatu wiki ijayo

KNUT yawataka walimu kufika shuleni kuanzia Jumatatu wiki ijayo

Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT kimewataka walimu kutii agizo la Tume ya Huduma za Walimu, TSC kwa kuanzia Jumatatu wiki ijayo.

Katibu Mkuu wa KNUT, Wilson Sossion tayari mikakati imewekwa ili kuhakikisha usalama wao wakati huu taifa linapokumbwa na janga la korona.

Wakati uo huo, Sossion amesikitishwa na idadi kubwa ya wanafunzi kupachikwa mimba tangu kuripotiwa kwa visa vya korona nchuini. Kwa mujibu wa Sossion, wanafunzi watakuwa salama skulini kulinganishwa na nyumbani.

Kwa upande wake Afisa wa Masuala ya Jinsia katika Hospitali ya Kenyatta, Alberta Wambu idadi kubwa ya visa vya dhulma vinahusisha mtoto wa kike hali inayohatarisha maisha yake.

Amesema asilimia kubwa ya mimba za mapema zinahusisha wanafunzi wa shule za msingi, huku zaidi ya visa 1,145 vikiripotiwa katika makazi ya watoto.

Wakati uo huo, Naibu Mwenyekiti wa KNUT Collins Oyuu amewataka wazazi kuwalinda wanao dhidi ya dhuluma katika jamii. Amewaonya kwamba watachukuliwa hatua za kisheria iwapo watashirikiana na wanaotekeleza maovu dhidi ya watoto wao.

Kwa mujibu wa TSC, walimu wa shule za msingi na upili watakuwa wa kwanza kuripoti shuleni Jumatatu.

Zaidi ya walimu elfu mia tatu themanini watafika shuleni ilikuanza matayarisho kuwapokea wanafunzi.

Aidha, wanafunzi wanaosomea kozi za sayansi na teknolojia wataripoti Jumatatu hiyo.
Juma lijalo, Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutangaza tarehe kamili ya wanafunzi kurudi shuleni baada ya kufanya kikao na washikadau wa sekta ya elimu na kamati ya kitaifa ya kudhibiti maambukizi ya Korona.