×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

PSC yamkosa Maraga kufuatia agizo la kuvunjwa kwa bunge

PSC yamkosa Maraga kufuatia agizo la kuvunjwa kwa bunge

Ushauri wa Jaji Mkuu, David Maraga kwa Rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge kufuatia kutoidhinishwa kwa mswada wa usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi unaendelea kuibua hisia nchini huku Tume ya Huduma za Bunge, PSC ikitishia kuwasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya Maraga.

PSC chini ya uwenyekiti wa Spika Justin Muruti  imelikosoa vikali  pendekezo la Jaji Mkuu, David Maraga la kulivunja bunge huku Muturi akisema tayari ameshauriana na mwenzake wa Bunge la Seneti kuwasilisha kesi katika mahakama Kuu kupinga ushauri huo wa Maraga. Amesema uamuzi wa Maraga haukuwa wenye busara na unalenga kuzua taharuki ya uongozi nchini.

Muturi ameelezea imani yake kwamba suala la bunge kukosa kuupitisha mswada wa uwakilishi sawa wa kijinsia linaweza kutatuliwa bila bunge kuvunjwa. Aidha, amesisitiza kwamba maamuzi ya mahakama yalilenga bunge lililotangualia na wala si la sasa.