×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais amsuta Naibu wake William Ruto kufuatia siasa za mapema

Rais amsuta Naibu wake William Ruto kufuatia siasa za mapema

Rais Uhuru Kenyatta amewasuta viongozi wanaoendeleza siasa za mwaka wa 2022 badala ya kuwahudumia Wakenya waliowachagua.

Katika kauli inayofikirika kumlenga Naibu wa Rais William Ruto na washirika wake , Rais Kenyatta amemtaja kuwa mbinafsi kwa kuendeleza siasa wakati ambapo taifa linakumbwa na janga la korona. 

Wakati uo huo, Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amewasuta viongozi wanaowatumia vijana katika kuzua vurugu.

Joho amemsuta Ruto kufuatia michango yake ya kila mara makanisani akiwalenga Wakenya wenye mapato ya chini

Kwa mujibu wa Joho, Ruto anafanya hivyo ili kuwahadaa kumpigia kura mwaka wa 2022, nakwamba kamwe hatapata uungwaji mkono kutoka kwa Wapwani.

Aidha, ameendelea kuwasuta viongozi wanaotoa semi za uchochezi akisema wanachochea uhasama miongoni mwa Wakenya.

Rais Kenyatta amewahakikishia wakazi wa Pwani kwamba mizozo ya ardhi itasuluhishwa. Pia amewaahidi kushughulikia malalamiko ya wafanyabiashara kufuatia hatua ya serikali kusafirisha bidhaa kutumia reli ya kisasa, SGR.