×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shughuli ya kuwahoji walimu ili kujaza nafasi za walimu elfu 11 kuanza wiki ijayo

Shughuli ya kuwahoji walimu ili kujaza nafasi za walimu elfu 11 kuanza wiki ijayo

Shughuli ya kuwahoji walimu ili kujaza nafasi za walimu elfu 11 zilizotangazwa zimeratibiwa kuanza wiki ijayo huku serikali ikiharakisha mchakato wa kurejelewa masomo. Walimu hao sasa huenda wakaihitajika shuleni mwezi ujao badala ya Janauri mwaka ujao siku chache kabla ya kufunguliwa kwa shule.

Wakurugenzi wa elimu katika kaunti wamejukumiwa kuweka ratiba ya mahojiano hayo, wengi wakisema watakamilisha shuhuli hiyo kabla ya shule kufunguliwa ili kuwezesha utekelezaji wa masharti ya kukabili korona.

Hayo yakijiri wakuu wa shuel za binafasi wameelezea ugumu wa kutekeleza baadhi ya masharti yaliyowekwa na serikali kabla ya shule kufunguliwa kutokana na ukosefu wa fedha. 

Kwa mujibu wa Naibu Mwenyekiti wa muungano huo Isaiah Mbaabu, serikali haijatoa mkopo wa shilingi bilioni 7 ilizoahidi.

Wazazi kwa upande wao wametakiwa kujitayarisha kugharamia masomo ya wanao hasa katika shule za binafsi. Akizungumza hapo jana Waziri Magoha, amewashauri wale hataweza kufanya hivyo kuwapeleka wanao katika shuel za umma