×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Tuju aitaka JSC kumuondoa Jaji Mary Kasango katika kesi inayomkabili

Tuju aitaka JSC kumuondoa Jaji Mary Kasango katika kesi inayomkabili

Mwenyekiti wa Chama cha Jubilee Raphael Tuju ameitaka Tume ya Huduma kwa Idara ya Mahakama, JSC kumuondoa Jaji Mary Kasango kutoka wadhifa huo wa Jaji wa Mahakama Kuu.

Tuju anamshutumu Kasango kwa kuwa na mapendeleo na kuegemea upande mmoja katika kesi dhidi yake ya deni la shilingi bilioni 1.5 analodaiwa na Benki ya East Africa Development.

Kiongozi huyo amesema kwamba Jaji Kasango amedhihirisha upendeleo na kuegemea upande wa benki hiyo kuulemea upande wa Dari Limited na wakurugenzi wake.

Katika kesi hiyo, benki hiyo inaitaka Mahakama kumshurutisha Tuju kulipa deni hilo ambalo alipewa mwezi Aprili 2015.