×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wizara ya Afya yathibitisha watu wengine105 kuambukizwa korona huku idadi ya waliofariki ikisalia kuwa

Wizara ya Afya yathibitisha watu wengine105 kuambukizwa korona huku idadi ya waliofariki ikisalia kuwa

Hakuna mtu aliyefariki kutokana na makali ya Ugonjwa wa Covid-19 leo hii.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Afya imesema idadi ya watu waliofariki kutokana na makali ya ugonjwa huo imesalia kuwa mia sita arubaini na sita, huku watu wengine mia moja na watano wakiambukizwa korona.

Idadi hiyo ni asilimia tatu nukta saba ya maambukizi baada ya sampuli elfu mbili, mia nane sitini na nane zilizopimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Kwa jumla watu elfu thelathini na sita, mia nane ishirini na tisa wameambukizwa virusi vya korona nchini humu tangu kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza mwezi machi mwaka huu.

Katika maambukizi hayo, watu themanini na watatu ni wa jinsi ya kiume huku ishirini na wawili wakiwa wa kike.

Miongoni mwa waliotangazwa kuambukizwa ni mtoto mchanga wa miaka miwili na mzee wa miaka tisini na mitano.

Aidha, wote ni Wakenya isipokuwa watu wawili ambao ni raia wa kigeni.

Kaunti ya Nairobi inaongoza katika maambukizi ya leo kwa kuwa na watu thelathini na watatu walioambukizwa, ambayo ni asilimia thelathini na moja ya maambukizim ya leo ikifuatwa na Busia kwa watu wengine kumi na watano ambayo ni asilimia kumi na nne, Mombasa asilimia nane baada ya watu tisa kuambukizwa, Bungoma watu wengine wanane ambayo ni asilimia saba nukta sita ya maambukizi ya leo, Kiambu, Nakuru, Taita Taveta, Bomet na Garissa zikirekodi watu wanne kila kaunti ambayo ni asilimia tatu nukta nane, Kakamega, Kisumu vilevile Kajiado zikirekodi watu watatu kila kaunti.

Aidha Kaunti za Machakos, Meru na Trans Nzoia zimethibitisha watu wengine wawili kila kaunti kuambukizwa korona huku Murang'a, Nyeri na Laikipia zikithibitisha mtu mmoja kila kaunti ambayo ni asilimia asilimia moja ya watu walioambukizwa leo hii.

Wakati uo huo watu wengine sitini na wanane wamepona Ugonjwa wa Covid-19, ambapo thelathini na wanane walikuwa wakihudumiwa wakiwa nyumbani huku waliokuwa kwenye hospitali mbalimbali wakiwa thelathini.

Kwa jumla watu elfu ishirini na tatu, mia saba sabini na saba wamepona ugonjwa  wa Covid-19 nchini.