×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shirika la Haki Africa laendesha ukaguzi wa fedha za korona katika Kaunti ya Mombasa

Shirika la Haki Africa laendesha ukaguzi wa fedha za korona katika Kaunti ya Mombasa

Ukaguzi wa matumizi ya fedha za kukabili janga la korona kwenye Kaunti ya Mombasa unaendelea. Shughuli hiyo inaendeshwa na Shirika la Kutetea Haki za Kibinadamu la HAKI Africa kwa ushirikiano na mashirika ya Amkeni Wakenya vilevile la Umoja wa Mataifa la Mipango na Maendeleo UNDP.

Ukaguzi huu unafanywa kwenye miradi yote iliyoanzishwa na Serikali ya Kaunti ya Mombasa katika juhudi za kukabili maambukizi zaidi tangu kisa cha kwanza cha korona mjini Mombasa kilipotangazwa.

Maafisa wa Haki Afrika waliopewa mafunzo ya jinsi ya kuendesha shughuli hiyo wamekuwa wakitembelea maeneo mbalimbali likiwmao eneo la Kivuko cha Likoni Feri ambapo kuna sehemu maalum ya kupuliza kemikali ya kuua viini kwa abiria kabla ya kuabiri Feri kuelekea ng'ambo ya pili.

Aidha ukaguzi huo unaleenga kubaini fedha zilizotumika katika kutengeneza eneo hilo vilevile idadi ya vitanda katika Hospitali ya Coast General na vipumuzi vilevile mavazi ya wahudumu wa afya wanaowahudumia wagonjwa wa Covid-19.

Kwa mujibu wa taarifa ya Haki Africa, maafisa wake watazuru Chuo cha Technical University of Mombasa kukagua sehemu iliyotengwa kuwashughulikia wagonjwa wa Covid-19, vilevile vitanda na vifaa vyote vilivyonunuliwa.

Aidha ukaguzi huo utafanyika katika kila Eneo Bunge kubaini idadi ya watu walionufaika na misaada mbalimbali kutoka kwa serikali ya kaunti wakati huu wa janga la korona kisha kulingishwa na kiwango cha fedha kilichotumika kufanikisha mpango huo.

Waziri wa Afya wa Kaunti ya Mombasa Hazel Koitaba amesema wameafikiana na mashirika hayo kufanya ukaguzi katika Sekta ya Afya na kisha kutoa ripoti yake. 

Katika kila eneo bunge, maafisa watano watawahoji wakazi mia tatu na hamsini katika kila eneo bunge kuhusu jinsi serikali ya kaunti hiyo inavyoendelea kukabili janga la korona maoni ambayo vilevile yatajumuishwa kwenye ripoti ya mwisho ambayo itakabishiwa washkadau wanaohusika katika vita dhidi ya korona.

Aidha utalenga kubaini utayarifu wa kaunti hiyo kukabili maambukizi hasa ikizingatiwa kwamba, hivi karibuni Kaunti ya Mombasa imekuwa ikirekodi idadi ya juu ya watu wanaoambukizwa virusi vya korona.

Hayo yanajiri huku ripoti ya madai ya wizi wa fedha za korona katika Mamlaka ya Kusambaza Dawa KEMSA ikikabidhiwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma DPP Noordin Hajj, ambayo iwapo itaidhinishwa basi wahusika wote kwenye ripoti hiyo watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.