×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 148 wamethibitishwa kuambukizwa korona nchini

Watu wengine 148 wamethibitishwa kuambukizwa korona nchini

Jumla ya watu elfu thelathini na sita, mia saba ishirini na wanne wameambukizwa virusi vya korona nchini humu.

Idadi hiyo imeongezeka baada ya watu wengine mia moja arubaini na wanane kuthibitishwa kuambukizwa virusi hivyo baada ya sampuli elfu mbili mia nne thelathini na nane kupimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Wizara ya Afya aidha imethibitisha kuwa watu wengine tisini na wanane wamepona ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha jumla ya watu waliopona ugonjwa huo kuwa elfu ishirini na tatu, mia saba na tisa.

Wakati uo huo, watu wanne zaidi wamefariki dunia kutokana na makali ya Covid-19 na kufikisha jumla ya watu waliofariki kuwa mia sita arubaini na sita.

Kufikia sasa jumla ya sampuli elfu mia tano kumi na moja, mia sita kumi na nne zimepimwa tangu kuthibitishwa kuwapo kwa virusi vya korona nchini.

Aidha, watu arubaini na sita miongoni mwa tisini na wanane waliopona walikuwa wakihudumiwa wakiwa nyumbani huku hamsini na wawili wakiwa kwenye hospitali mbalimbali.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya maambukizi ya leo ni wanaume mia moja na watano na arubaini na watatu wa jinsia ya kike huku mchanga zaidi akiwa wa umri wa miaka miwili. Aidha watu watatu pekee miongoni mwa mia moja arubaini na wanane waliothibitishwa kuambukizwa ni raia wa kigeni wanaoishi nchini.

Katika maambukizi yaliyotangazwa leo, Kaunti ya Mombasa inaongoza kwa kuwa na idadi ya juu ambapo watu arubaini wameambukizwa, ikifuatwa na Nairobi kwa watu thelathini na wawili, Laikipia kumi na watano, Kiambu kumi na mmoja, Nakuru na Embu zikiwa na watu saba saba walioambukizwa kisha Kajiado na Uasin Gishu zikiwa na watu sita sita walioambukizwa leo hii.

Kaunti ya Taita Taveta imeripoti watu watano vilevile Kisumu, Kitui watu wanne walioambukizwa korona, Baringo, Elgeyo Marakwet, Kwale, Machakos, Kericho, Makueni na Muarang'a zikithibitisha mtu mmoja kila kaunti kuambukizwa korona.

Wizara ya Afya aidha imeendelea kuwahimiza Wakenya kufuata maagizo yaliyowekwa ili kufanikisha vita dhidi ya janga la korona.