×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

LSK imeishtaka serikali kwa kuweka usimamizi wa KMC chini ya Wizara ya Ulinzi

LSK imeishtaka serikali kwa kuweka usimamizi wa KMC chini ya Wizara ya Ulinzi

Chama cha Wanasheria, LSK kimewasilisha ombi la dharura mahakamani kupinga uamuzi wa serikali kuweka Kampuni ya Nyama, KMC chini ya usimamizi wa Wizara ya Ulinzi.

Uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta kuhusu suala hilo, lilitolewa na Waziri wa Kilimo Peter Munya kupitia agizo la rais hatua ambayo inaendelea kuibua mjadala mkali nchini hasa miongoni mwa wanasiasa.

LSK  kupitia wakili Hosea Omanwa imewasilisha ombi hilo mahakani ikitaja hatua ya Kenyatta kuwa kinyume na sheria.

Chama hicho kimesema kwama KMC ni taasisi ya serikali yenye majukumu yake yanayolindwa kisheria na hivyo basi kuihamisha katika Wizara ya Ulinzi ni ukiukaji mkubwa wa kifungu 383 ya katiba

Jaji Anthony Mrima amelitaja ombili hilo kuwa la dharua huku akiagizwa  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kihara Kariuki na Waziri wa Kilimo Peter Munya kushughulia malalamiko ya LSK chini ya kipindi cha wiki moja.

Mrima amewaagiza washtakiwa kujibu malalamiko ambayo yamewasilishwa mahakani chini ya siku kumi kuiwezesha mahakama kuanza kuskiza ombi hilo.

Maseneta wiki hii wamekuwa wakiendeleza shutma kali dhidi ya uamuzi huo na hata mara si moja kutumia vikao vya alasiri kupinga uamuzi wa Kenyatta ambao unalenga kuboresha shughuli za KMC