×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi aachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi aachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano

Mahakama imemwachilia kwa dhamana ya shilingi elfu mia tano pesa taslimu Mbunge wa Kapsaret Oscur Sudi anayekabiliwa na mashtaka matano yakiwamo ya uchochezi.

Mahakama imemwagiza mbunge huyo dhidi ya kutoa taarifa zozote umma kuhusu mashtaka yanayomkabili .

Akitoa uamuzi huo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Nakuru,  Joel Ngugi  amesema hakuna sababu za kimsingi za  kuendelea kumzuilia Sudi.

Ikumbukwe, ombi la kutaka Sudi aachiliwe liliwasilishwa  na baadhi ya wabunge kupitia kwa mawakili wa Sudi wakitaka aachiliwe baada ya mahakama siku ya Jumanne wiki hii kuagiza azuiliwe rumande kwa siku nyingine saba hadi kesi ya uchochezi dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa wakisema uamuzi huo haukufaa.

Wakati wa kikao cha asubuhi, Sudi ameieleza mahakama kwamba hatatoa matamshi yoyote ya uchochezi atakapoachiliwa huru na kwamba atadumisha amani akisubiri kuendelea kwa kesi dhidi yake. Ikumbukwe Sudi alifunguliwa mashtaka akihusishwa na matamshi ya kumkosea heshima Rais Uhuru Kenyatta na familia yake.