×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baraza la Magavana limeondoa tangazo la kusitisha huduma kwa kaunti

Baraza la Magavana limeondoa tangazo la kusitisha huduma kwa kaunti

Baraza la Magavana limeagiza kurejelewa kwa huduma zote za serikali za kaunti siku moja tu baada ya Bunge la Seneti kuidhinisha mfumo mpya wa ugavi wa fedha za kaunti.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Wycliffe Oparanya amewaagiza magavana kuhakikisha shughuli zote zinarejelea kwani sasa kuna matumaini ya kaunti zote kupokea mgao wao wa pesa.

Juzi Oparanya ambaye pia ni Gavana wa Kakamega, aliwaagiza magavana kusitisha huduma za kaunti kutokana na ukosefu wa fedha baada ya maseneta kushindwa mara kumi kuidhinisha mfumo huo.

Tangazo la Oparanya limejiri saa chache tu baada ya Waziri wa Fedha Ukur Yattani kusema Kaunti zitapokea mgao wa shilingi bilioni 60 kufikia Jumatatu ijayo.

Aidha, Yatani amesema fedha hizo ni sehemu ya shilingi  bilioni 316. 5 za mgao wa kaunti kwenye bajeti ya mwaka wa kifedha 2020-2021.

Wakati uo huo Waziri Yatani amewahakikishia Wakenya kwamba fedha hizo zitafika kwa serikali za kaunti siku ya Jumatatu ili kufanikisha shughuli za maendeleo mashinani baada ya kuathiriwa  kutokana na ukosefu wa fedha.

Waziri amesema anatarajia Rais Uhuru Kenyatia kuidhinisha kusambazwa kwa fedha hizo leo hii.

Jana maseneta kwa kauli moja waliafikiana kupitisha mfumo ambao utazinufaisha kaunti zote kwa usawa ambapo maseneta 41 walipiga kura ya ndio na kupitisha mapendekezo ya kamati ya maseneta kumi na wawili iliyoteuliwa kutafuta mwafaka huo.

Mfumo huo utahakikisha kuwa kaunti zinapewa shilingi bilioni 370 kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kabla ya kubadilishwa.