×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Marufuku ya michezo yote kuendelea kwa mwezi mmoja

Marufuku ya michezo yote kuendelea kwa mwezi mmoja

Marufuku ya michezo yote inayowashirikisha wachezaji wasiozidi umri wa miaka kumi na minane vilevile ile ya soka, voliboli, ndondi na mchezo wa kuogelea yataendelea kuwapo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Michezo Balozi Amina Mohamed michezo hiyo itaendelea kusitishwa kwa muda wa mwezi mmoja kwa kuwa wachezaji hukaribiana wanapokuwa uwanjani na hivyo kuwaweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya korona.

Akizungumza wakati wa kuzindua mwongozi wa kufanikisha kurekelewa kwa shughuli za kichezo, Amina amesema mwongozo huo utabadilishwa kulingana na hali ya maambukizi huku akisisitiza haja ya sheria zilizowekwa na Wizara ya Afya kufuatwa wakati wa michezo mbalimbali.

Hata hivyo maeneo ya kufanyia mazoezi vilevile vilabu vya binafsi ambavyo vimeafikia mwongozo huo vinaweza kurejelea shughuli japo kwa kuzingatia masharti makali.

Uzinduzi wa mwongozo huu unajiri baada ya ripoti ya kufanikisha kurejelewa kwa shughuli za michezo kutolewa ambapo washikadau walitoa maoni yao kabla ya kuwekwa wazi leo.