×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Familia 600 mtaani Majengo zapewa msaada wa chakula kupitia mpango wa I Stand With Kenya

Familia 600 mtaani Majengo zapewa msaada wa chakula kupitia mpango wa I Stand With Kenya

Zaidi wa familia mia sita zisizojiweza katika Mtaa wa Majengo jijini Nairobi zimenufaika na msaada wa chakula kupitia mpango wa Shirika la Habari la Standard Group, PLC na washirika wengine kwa jina I Stand With Kenya kuziwezesha kujimudu wakati huu wa maambukizi ya janga la korona.

Familia hizo zikijumuisha watu wenye ulemavu, akina-mama wajane, waliodhulumiwa na vijana wasiokuwa na ajira zimepokea msaada huo wa chakula huku zikiipongeza Shirika la Standard Group, PLC na wafadhili wake kwa kuwajali wakati huu wa maambukizi ya korona.

Shirika hili limetoa hakikisho la kuendelea kuwapa Wakenya msaada kwa ushirikiano na washirika wengine huku likiwapongeza wafadhili ambapo wamesaidia pakubwa kufanikisha malengo ya mradi huo ambapo kufikia sasa zaidi wa familia elfu ishirini na tano zimepewa msaada wa chakula.

Shirika la Standard Group, PLC liliwakilishwa na Jan Mohammed mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi

Baadhi ya washirika wa mradi huo ulioanzishwa miezi mitatu iliyopita kwa lengo la kuwasaidia wasiojiweza kutokana na janga la korona ikiwamo Kampuni ya Bima ya APA na Shirika la Msalaba Mwekundu wamesema wataendelea kuweka mikakati ya kuwafikia watu wengi zaidi wanaohitaji msaada wakati huu.

Standard Group inalenga kupanua mradi huo ili kuwafikia watu wengine nchini ikiwa njia mojawapo ya jukumu la kampuni hii kushughulikia maslahi ya umma na kuchangia ukuaji wa uchumi.