×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta azindua utengenezaji wa madawati yatakayotumiwa shuleni

Rais Kenyatta azindua utengenezaji wa madawati yatakayotumiwa shuleni

Rais Uhuru Kenyatta mapema leo amezindua rasmi mradi wa kutengeneza madawati ya kima cha shilingi milioni 1.9 jijini Nairobi.

Mradi huo utafanikisha kusambazwa kwa madawati takriban elfu mia sita hamsini kwa shule za msingi na upili nchini .

Rais amezindua mradi huo katika hafla ambayo imehudhuriwa na Waziri wa Elimu Profesa George Magoha na Katibu wa Wizara ya Usalama wa Ndani Karanja Kibicho katika eneo la Umoja.

Kenyatta amesema kuwa mradi huo ni sawa na ule wa Kazi Mtaani ambao unalenga kuwapa uwezo wa kiuchumi vijana hasa wakati huu mgumu wa maambukizi ya korona.

Rais vilevile, amewahamikikisha vijana kwamba serikali yake itaendelea kuweka mikakati ya kuwapa ajira hasa wale wanaofuzu katika nyanja mbalimbali

Katika bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2020-2021 sekta ya elimu ilipewa mgao mkubwa wa shilingi bilioni 2.1 ambapo bilioni 1.9 zilitengewa mradi huo wa madawati.

Kando na kusambaza madawati, mradi huo pia utapiga jeki sekta ya jua kali ambapo vijana hasa wamelengwa katika kutengeneza madawati hayo.