×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hatimaye maseneta wapitisha mfumo wa ugavi wa mapato ya kaunti

Hatimaye maseneta wapitisha mfumo wa ugavi wa mapato ya kaunti

Hatimaye vuta ni kuvute katika Seneti kuhusu ugavi wa mapato kwa kaunti imefika kikomo. 

Maseneta arubaini na mmoja wamepiga kura kuyapitisha marekebisho ya mapendekezo ya mswada huo huku kukiwa hakuna hata mmoja ambaye amepiga kura kupinga. Kupitishwa kwa ripoti hiyo sasa kutoa nafasi kwa Hazina Kuu ya Kitaifa kusambaza fedha kwa kaunti mbalimbali.

Shughuli ya kupiga kura imeanza muda mchache baada ya kusomwa kwa ripoti ya Kamati ya Maalum ya Maseneta kumi na wawili. Kinyume na ilivyokuwa kwenye vikao vya awali, Spika Ken Lusaka amekuwa mwenye tabasabu huku mara si moja Seneta Silvyia Kasanga akisema maseneta wote wanaunga mkono ripoti hiyo.

Aidha Seneta wa Kakamega Clophas Malala wa Kilifi Steward Madzayo, wa Makueni Mutula Kilonzo Junior ,wa Elgeiyo Marakwet Kipchumba Murkomen ambao wamekuwa wakipinga mfumo huo, wamekuwa mwenye furaha na kupiga kura kuunga mkono mswada huo.

Ugavi wa fedha kwa kaunti sasa utazingatia vipengelea mbalimbali vikiwamo viwango vya umaskini kwenye kaunti, kilimo na ufugaji, uchumi wa kila kaunti, sekta ya afya vilevile maendeleo ya miji kwenye kaunti mbalimbali. Kwa kauli moja maseneta wamesema kuwa mswada huo utahakikisha kila kaunti haipotezi mgao wake wa fedha.