×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 183 waambukizwa virusi vya korona nchini Kenya

Watu wengine 183 waambukizwa virusi vya korona nchini Kenya

Watu wengine mia moja themanini na watatu wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita baada ya kupimwa kwa sampuli elfu nne mia moja themanini na nane. 

Wote walioambukizwa ni Wakenya isipokuwa kumi na wanne ambao ni raia wa kigeni. Mtoto mchanga wa umri wa miezi saba na mzee mwenye umri wa miaka themanini ni miongoni mwa walioambukizwa.

Katika idadi hiyo, mia moja thelathini na mmoja ni wanaume huku wanawake wakiwa hamsini na wawili. Wengi wa walioambukizwa wako jijini Nairobi ambapo watu hamsini na wanne wameathirika. Daktari Mercy Mwangangi ni Katibu wa Utawala katika Wizara ya Afya.

Aidha, wahudumu wa afya takriban mia tisa arubani na watano wameambukiziwa virusi vya korona humu nchini tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza huku kumi na sita wakifariki dunia.

Wakati uo huo, watu wengine themanini na wawili wamepona baada ya kuambukizwa virusi vya korona ambapo arubaini na tisa miongoni mwao ni wale waliokuwa wakihudumiwa hospitalini huku thelathini na watatu wakiwa wale wa nyumbani.

Idadi jumla ya waliopona sasa imefika elfu ishirini na tatu, mia sita kumi na mmoja. Hata hivyo, watu wengine watano wamefariki dunia na kufikisha idadi jumla ya vifo kuwa mia sita arubaini na viwili.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika Wizara ya Afya, Daktari Partrick Amoth amesema Kenya i tayari kukumbatia chanjo mbalimbali ambazo zitaidhinishwa kukabili korona japo amewashauri wananchi kuendelea kuzingatia masharti ya kukijinga kwani kufikia sasa bado tiba haijapatikana.