×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waiguru na wawakilishi wadi wa Bunge la Kirinyaga wazika tofauti baina yao

Waiguru na wawakilishi wadi wa Bunge la Kirinyaga wazika tofauti baina yao

Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru ameafikiana kufanya kazi na wawakilishi wa wadi baada ya mvutano kati yao kushuhudiwa.

Waiguru na wawakilishi hao wameafikia kuanzisha mpango wa ujenzi wa kilomita mia mbili arubaini ya barabara kuanzia Januari mwakani.

Haya yanajiri baada mazungumzo yaliyoongozwa na Muungano wa Mt.Kenya katika harakati za kutafuta mwafaka baina ya gavana huyo na wawakilishi wadi.

Waiguru amewaahidi kuondoa kesi aliyowasilisha mahakamani kuwashtaki wawakilishi hao baada ya kukataa kupitisha bajeti ya kaunti.

Ikumbukwe wawakilishi wadi hao walikuwa wamepiga kura ya kumng'atu Waiguru mamlakani ila akanusuriwa na seneti.

Gavana huyo alishtumiwa kufuatia uporaji wa fedha za kaunti, utumizi mbaya wa ofisi, vilevile kutofuata sheria wakati wa kutoa tenda.