×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kamati ya Seneti yapata mwafaka kuhusu mfumo wa ugavi wa fedha za kaunti

Kamati ya Seneti yapata mwafaka kuhusu mfumo wa ugavi wa fedha za kaunti

Kamati Maalum ya Maseneta kumi na wawili iliyotwikwa jukumu la kuangazia mfumo wa ugavi wa mapato imepata mwafaka kuhusu mgogoro wa mswada mpya wa ugavi wa mapato kwenye serikali za kaunti.

Kwa mujibu wa Spika Ken Lusaka, ripoti hiyo itawasilishwa baadae leo katika seneti kujadiliwa na kisha kupigiwa kura.

Awali maseneta Mutula Kilonzo Junior wa Makueni na mwenziwe wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kupitia mitandao ya kijamii walidokeza kuwa wako karibu kupata mwafaka baada ya kikao cha leo kilichoanza mapema asubuhi.

Iwapo maseneta watapigia kura kupitisha mapendekezo ya ripoti hiyo basi itasaidia kukwamua huduma mbalimbali za kaunti mashinani ambapo tayari Magavana wametishia kusitisha baadhi ya huduma zikiwamo za afya kutokana na ukosefu wa fedha.

Ikumbukwe seneti imeahirisha vikao vyake kuhusu mswada huo tata kwa mara ya kumi  sasa, huku bunge likigawanyika kwenye makundi mawili lile linaloounga mkono kutumika kwa mapendekezo ya Tume ya Ugavi wa Mapato CRA ya kutumia idadi ya watu na lile linaloshinikiza kuwapo kwa usawa kwa kutumia ukubwa wa eneo.