×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Chama cha Wauguzi, KNUN chawashtumu maseneta kufuatia mvutano wa muda mrefu kuhusu ugavi wa mapato

Chama cha Wauguzi, KNUN chawashtumu maseneta kufuatia mvutano wa muda mrefu kuhusu ugavi wa mapato

Bunge la Seneti limeshtumiwa vikali kwa mvutano ambao umekuwa ukiendelea kuhusu mfumo wa ugavi wa fedha za kaunti hali ambayo imechangia tangazo la Baraza la  Magavana kusitisha huduma kwenye kaunti zote kufuatia ukosefu wa fedha. Chama cha Wauguzi nchini, KNUN kimewashtumu maseneta kwa kutoyajali maslahi ya wananchi na badala yake kuendelea kuzozana kuhusu mfumo wa ugavi wa fedha.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Seth Panyako amesema maseneta wametumia muda mwingi kujadili suala hilo kwa kuwa ilivyo sasa wanaendelea kupokea mishahara yao hivyo hawajaathiriwa na ukosefu wa fedha jinsi inavyofanyika kwa wafanyakazi wa kaunti.

Panyako amependekeza katiba ifanyiwe marekebisho ili Tume ya Huduma za Afya ibuniwe na ambayo itahakikisha kwamba fedha za wahudumu wa afya zinalipwa moja kwa moja katika akaunti zao badala ya kuelekezwa kwanza kwa kaunti kisha kuwalipa.

Wakati uo huo,  amelishtumu Bunge la Kitaifa kwa kutopitisha sheria ya kuhakikisha asilimia 50 ya fedha inatumwa kwenye kaunti kwa kuzingatia mfumo uliotumika katika mwaka wa kifedha uliotangulia ili kuhakikisha huduma zinaendelea kwenye kaunti.

Hapo jana  Waziri wa Fedha, Ukur Yatani alisema kwamba hana mamlaka ya kutoa mgao wa asilimia hamsini katika serikali za kaunti hadi pale atakapopata idhini ya bunge