×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hatua ya Mahakama kuagiza kuendelea kuzuiliwa kwa Oscur Sudi si kiinyume na sheria

Hatua ya Mahakama kuagiza kuendelea kuzuiliwa kwa Oscur Sudi si kiinyume na sheria

Hatua ya Mahakama kuagiza kuendelea kuzuiliwa kwa Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi inaendana na sheria. Haya ni kwa mujibu wa Wakili Alutalala Mukwana ambaye amesema kamwe hajadhulumiwa.

Kulingana na Mukwana, baada ya Sudi kuwasilishwa katika Mahakama ya Nakuru mbele ya Hakimu Joseph Kalu kwa mara ya pili na kisha kutoa uamuzi wa kuzuiliwa kwa siku nyingine saba, ilichangiwa na ombi la upande wa mashtaka na kwamba upo katika mkondo wa sheria.

Akizungumza na Radio Maisha Mukwana amesema mahakama ina uwezo wa kutoa uamuzi wa kuendelea kuzuiliwa kwa mshukiwa baada ya kufunguliwa mashtaka jinsi ilivyofanyika kwa Sudi, kwa kuwa alifikishwa mahakamani mara ya kwanza na kukabiliwa na mashtaka matano likiwamo la uchochezi, hivyo basi uamuzi wa mahakama unaambatana na sheria.

Baada ya siku saba kukamilika, Sudi aterejeshwa mahakamani na kujua iwapo ataachiliwa kwa dhamana au la. Kwa sasa Sudi anaendelea kuzuiliwa korokoroni, huku mawakili wake akiwamo Gladys Boss Shollei ambaye vilevile ni Mwakilishi wa Kike wa Uasin Gishu, na Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen wakipinga vikali uamuzi wa mahakama, akidai kwamba si haki kuendelea kumzuilia Sudi.