×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakazi wa Makueni waziiba bidhaa za padre baada ya gari lililokuwa likizisafirisha kuhusika katika ajali

Wakazi wa Makueni waziiba bidhaa za padre baada ya gari lililokuwa likizisafirisha kuhusika katika ajali

Kizaazaa kimeshuhudiwa kwenye soko la Mbui Nzau katika Kaunti ya Makueni kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi wakati gari moja lililokuwa likisafirisha mali ya padre moja kuanguka huku wakazi wakiiba vifaa vya kufanya misa, mavazi ya padre, divai pamoja na vifaa vya nyumbani vikiwamo vitanda na vitu vya kielektroniki.

Aaron Ngolania ambaye pia ni kiongozi wa kanisa, alishuhudia kisa hicho na kuwahimiza wote walioba bidhaa za padre kuzirejesha.

Amewashukuru wote walioamua kurejesha mali walioiba akisema si vyema kuiba mali ya mtu aliyehusika katika ajali ila cha muhimu ni kumsaidia.