×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maseneta wakashifu hatua ya kaunti kutangaza kusitisha huduma

Maseneta wakashifu hatua ya kaunti kutangaza kusitisha huduma

Maseneta wamelishtumu Baraza la Magavana kwa kutoa agizo la kusitishwa kwa huduma za kaunti na kuwataka magavana kutolitii agizo hilo. Beatrice Maganga ana taarifa zaidi.

Wakizungumza katika kikao cha alasiri cha bunge, maseneta wamelitaja agizo hilo kuwa ukiukaji mkubwa wa sheria lisilozingatia haki za wananchi ambao wataathirika pakubwa endapo huduma za kaunti zitasitishwa.  Wamesema magavana watawajibishwa moja kwa moja endapo vifo vitashuhudiwa kwenye kaunti kufuatia kusitishwa kwa huduma za matibabu.  Miongoni mwa maseneta waliozungumzia suala hilo ni Johnstone Sakaja wa Nairobi, Mutula Kilonzo Junior wa Makueni, Ledama

Maseneta aidha wamemshtumu Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Wyclif Oparanya kwa kuwaagiza wafanyakazi wote wa kaunti kwenda kwa likizo ya lazima wakisema hana mamlaka dhidi ya wafanyakazi hao. Wameikosoa tajriba ya Oparanya katika utendakazi wake wakisema ameonesha kutofaa kuhudumu katika wadhifa huo na hata kumlinganisha na watangulizi wake ambao maseneta wamewataja kuwa waliokuwa waadilifu katika utendakazi wao.  

Aidha wamesema ni kinaya kwa gavana huyo kuhudhuria kikao cha Rais Uhuru Kenyatta cha kujaribu kutafuta suluhu kuhusu ugavi wa fedha za kaunti kisha saa chache baadaye kutoa maagizo yanayokoshea heshima yaliyoafikiwa wakati wa kikao cha Rais.

Ikumbukwe maseneta kwa upande wao wameishindwa kuupitishwa mswada wa ugavi wa fedha za kaunti takriban mara kumi kufuatia mivutano baina yao japo wanasisitiza kwamba mwafaka utapatikana.