×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Shughuli za kaunti kusitishwa kuanzia kesho kufuatia ukosefu wa fedha

Shughuli za kaunti kusitishwa kuanzia kesho kufuatia ukosefu wa fedha

Baraza la Magavana limetangaza kusitishwa kwa shughuli zote za kaunti kuanzia kesho. Akitoa tangazo hilo, Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya aidha amewataka magavana kutoa ilani ya kuwatuma wafanyakazi katika likizo ya lazima kwa muda wa wiki mbili.

Aidha, baraza hilo limeagiza kutoruhusiwa wagonjwa wapya katika hospitali za umma huku akiwasihi Wakenya kutafuta huduma za matibabu kwenye hospitali za binafsi.

Baraza hilo linalaumu seneti kwa kutopitisha mswada wa fedha hata baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutoa shilingi bilioni hamsini na tatu katika mwaka ujao wa kifedha.

Wakati uo huo, Gavana wa Laikipia Nderitu Muriithi amesema kusitishwa kwa shughuli zote katika serikali za kaunti kutasababisha kukwama kwa miradi ya maendeleo.

Amewasuta maseneta na serikali kwa kuhujumu ugatuzi, huku akiitaja kuwa janga kubwa nchini.

Haya yanajiri huku Waziri wa Fedha, Ukur Yatani akisisitiza kwamba hana mamlaka ya kutoa mgao wa asilimia hamsini katika serikali za kaunti hadi pale atakapopara idhini ya bunge.

Yatani ambaye amefika mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Fedha, aidha amesema anawasubiri maseneta kupitisha mswada wa mapato ya kaunti.

Ikumbukwe maseneta wamekosa kupitisha mswada huo kwa mara kumi sasa, hali ambayo inazidi kulemaza shughuli za maendeleo nchini.