×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya imepokea shehena ya vifaa vya matibabu kutoka Qatar huku ikirekodi visa 92 vya korona

Kenya imepokea shehena ya vifaa vya matibabu kutoka Qatar huku ikirekodi visa 92 vya korona

Juhudi za kukabili maambukizi ya virusi vya korona zimepigwa jeki humu nchini, baada ya serikali kupokea shehena ya vifaa vya matibabu kutoka kwa taifa la Qatar huku Kenya leo hii  ikirekodi asimilia 3.0 ya maambukizi ya virusi vya korona.

Kando na korona, Serikali ya Kitaifa imesema imeweka mikakati ya kutekeleza kikamilifu mradi wa afya bora kwa wote UHC.

Wizara ya Mashauri ya Nchi za kigeni imeikabidhi serikali shehena ya vifaa vya matibabu vitakavyofanikisha kukabiliwa kwa janga la korona. Vifaa hivyo vinajumuisha vitanda vya wagonjwa mahututi, vipumuzi, barakoa na kemikali za kuu vinii miongoni mwa vifaa vingine.

Katibu wa Utawala katika Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni Ababu Namwamba ameikabidhi Wizara ya Afya vifaa hivyo.

Ababu ameishukuru Serikali ya Qatar kwa kuwapa msaada Wakenya waliokwama nchini humu wakati taifa hilo lilipositisha safari za ndege kutokana na janga la korona.

Msaada huu umejiri huku Kenya ikiripoti visa tisini na viwili vya maambukizi ya korona kutokana na sambuli 2,985 na sasa kufikisha idadi jumla ya visa kuwa elfu thelathini na sita, mia tatu sitini na vitatu.

Waliombukizwa, wanne ni raia wa kigeni huku themanini na wanane wakiwa Wakenya.Walioambukizwa sitini na wanne ni wanawake huku ishirini na wanane wakiwa wa kiume. Mtu mdogo zaidi ana umri wa miaka miwili huku mkubwa akiwa na umri wa miaka sabini na mitano.

Dakta Mercy Mwangangi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya

Kaunti za Nairobi na Mombasa zinaendelea kuongoza kwa visa vya maambukizi humu nchini huku Wizara ya Afya ikiendelea kusisitiza umuhimu wa Wakenya kujilinda.

Aidha watu mia moja sitini na watano wamethibitishwa kupona Covid-19 , sitini wakiwa wale wa nyumbani huku mia moja na watano wakiwa waliokuwa wakihudumiwa hospitalimi.

 Hata hivyo, watu wengine watatu wamefariki na kufikisha idadi jumla kuwa 637

Wakati uo huo, Wizara ya Afya imesema inaendelea kuweka mikakati ya kutekeleza mpango wa huduma bora ya afya kwa wote UHC ili kulinda afya ya Wakenya licha ya janga la korona.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dakta Mercy Mwangangi amesema serikali inaweka mfumo wa kuhakikisha pana fedha za kukabili majanga mbalimbali na kuwalinda raia.

Mwangangi aidha amesema kufikia sasa serikali imewanufaisha zaidi ya watu elfu mbili na huduma za afya bila malipo wakiwamo wazee na wanaougua magonjwa sugu.