×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Utata waibuka kuhusu idadi kamili ya waumini wa Legio Maria waliofariki kufuatia makabiliano

Utata waibuka kuhusu idadi kamili ya waumini wa Legio Maria waliofariki kufuatia makabiliano

Utata unaendelea kuzingira idadi kamili ya waumini wa dini ya Legio Maria waliofariki dunia kufuatia makabiliano makali baina ya pande mbili hasimu katika eneo la kuabudu la Got Kwer katika Kaunti ya Migori.

Maafisa wa polisi tayari wamefunga eneo hilo hapo jana na kusema kwamba idadi ya watu waliofariki dunia ni watano.

Kamanda wa Polisi wa Migori Manase Musyoka amesema kwamba waumini wawili walifariki dunia papo hapo huku wengine watatu wakifariki baadaye hospitalini kufuatia makabilioni hayo kuhusu uongozi wa dini hiyo. Hata hivyo, Kundi linaloongozwa na Papa Raphael Adika limedai kwamba watu kumi na wawili wamefariki dunia huku wawili wakiwa hawajulikani walipo.

Inadaiwa kwamba kundi lililokuwa limeondoka kanisani humo likiongozwa na Adika lilijitokeza katika sherehe za makumbusho ya mwanzilishi wa dini hiyo Melkio Ondeto na kuanza kuwarushia mawe wenzao chini ya uongozi wa Papa Laurence Kalul.

Wawili hao wamekuwa wakizozania uongozi tangu kufariki dunia kwa Ondeto.

Kundi la Adika baadaye lilikabiliana na polisi waliofika kutuliza hali huku ikidaiwa kuwa kuna baadhi ya polisi waliojeruhiwa.

Mzozo umekuwa ukitokota kwa muda baina ya viongozi wawili masimu Raphael Adika na Laurence Kalul.