×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Tanzania imeondoa marufuku ya kutua kwa ndege za Kenya Airways nchini humo

Tanzania imeondoa marufuku ya kutua kwa ndege za Kenya Airways nchini humo

Taifa la Tanzania limeondoa marufuku ya kutua kwa ndege za Shirika la Kenya Airways nchini humo.

Marufuku hayo yameondolewa siku moja tu baada ya serikali ya Kenya kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, KCAA, kutangaza kwamba raia wa Tanzania hawatashurutishwa kuwekwa karantini ya siku 14 baada ya kuwasili humu nchini kutokana na hofu maambukizi ya virusi vya korona.

Hii ni awamu  ya tatu ambapo Kenya imefungua anga zake kwa safari za ndege za kamataifa baada ya kufungwa kufuatia janga la korona mapema mwezi Machi mwaka huu.

Mataifa mengine ambayo yameongezwa katika orodha hiyo ni Ghana, Nigeria, na Sierra Leone. Ikumbukwe kuwa Kenya ilirejelea safari zake za ndege za kimataifa Agosti tarehe mosi kwa mataifa kumi na moja pekee ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona.

Agosti 19, orodha ya mataifa yaliongezwa na kufikia 130 japo Tanzania ikafungiwa nje tena huku serikali ikisema kwamba itaendelea kuongeza idadi ya mataifa kutokana na hali ya maambukizi.

Hatua ya Kenya kuitema Tanzania ilizidisha uhasama ambao umekuwapo kwa muda huku madereva wa matrela wa Kenya wakilazimika kupimwa mara mbili kabla ya kuingia Tanzania na hata wengine kuzuiwa kuingia nchini humo..