×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakazi 300 wa Kawangware wamenufaika na chakula kupitia mradi wa I stand with Kenya

Wakazi 300 wa Kawangware wamenufaika na chakula kupitia mradi wa I stand with Kenya

Takriban familia zaidi ya mia tatu katika Mtaa wa Kawangware jijini Nairobi zimenufaika na msaada wa chakula kuzisaidia wakati huu mgumu wa makali ya janga la korona.

Msaada huo wa chakula umetolewa kupitia mradi wa Shirika la Habari la Standard Group PLC,  kwa jina I Stand with Kenya kwa ushirikiano na washirika mbali mbali.

Wakazi hao wakiwamo wakongwe, akinamama na vijana wameipongeza Shirika hili kwa kuanzisha mradi huo.

Mradi huo ambao ulianzishwa miezi mitatu iliyopita kuwapa afueni familia zisizojiweza hasa kwenye mitaa ya mabanda umezifaidi zaidi ya familia elfu saba tangu kuanzishwa kwake.

Esther Musyoki aliyeiwakalisha Shirika la Standard Group, PLC wakati wa hafla hiyo, amesema kwamba kufikia sasa kampuni imeafikia lengo ya mradi huo ambapo awali walikusudia kuzipa msaada familia mia saba kwa siku.

Baadhi ya wafadhili wa mradi huo wamefurahishwa na hatua zilizopigwa kufikia sasa kuwapa msaada wasiojiweza katika Jamii wakati huu mgumu.

Mratibu wa kibiashara katika Kampuni ya Premier Food Industries Limited Kevin Osunga amesema kuwa wanalenga kuzifikia familia nyingi hata zaidi jijini Nairobi.

Siku ya Ijumaa wiki hii, wakazi wa majengo watakuwa wakinufaika na msaada wa chakula kupitia mradi huo wa I Stand with Kenya.