×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Babu Owino asitisha maandamano yaliopangwa kulalamikia kutolipwa kwa walimu wa bodi za shule

Babu Owino asitisha maandamano yaliopangwa kulalamikia kutolipwa kwa walimu wa bodi za shule

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amesitisha maandamano yaliyopangwa kulalamikia kutolipwa kwa walimu walioajiriwa na bodi za shule. Hatua hiyo ni baada ya walimu hao kukiri kuanza kupokea mishahara waliyoahidiwa miezi miwili iliyopita kuanzia hapo jana.

Kwa muda sasa, walimu hao wamekuwa wakilalamikia kutotimizwa kwa agizo hilo lililotolewa na Rais Uhuru Kenyatta vilio ambavyo tulipeperusha mara si moja hapa Radio Maisha.

Hata hivyo, Jumatatu, Waziri wa Elimu Prof George Magoha alisisitiza fedha zilikuwa zimetolewa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Kadhalika aliahidi kuhakikisha wafanyakazi wengine kama vile walinzi pia wanalipwa.

Kufikia hapo jana, walimu kadhaa walikuwa wameanza kupokea fedha hizo.

Share this: