×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wafanyabiashara wa Nairobi Railways Club wakadiria hasara kufuatia ubomoaji wa vibanda vyao

Wafanyabiashara wa Nairobi Railways Club wakadiria hasara kufuatia ubomoaji wa vibanda vyao

Wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Nairobi Railways Club wanaendelea kukadiria hasara baada ya vibanda vyao kubomolewa usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa kwamba matingatinga ya serikali yaliwasili eneo hilo usiku wa kuamkia leo chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi ambao kufikia sasa wangali wameshika doria.

Ubomozi huo unajiri saa chache tu baada ya Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika la Reli Nchini Pharis Ngotho kuwapa wafanyabiashara hao notisi ya saa nane kuondoka eneo hilo ili kupisha ujenzi wa barabara ya moja kwa moja kuanzia uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta kuelekea Westlands.