×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Waziri Yatani aelezea uwezekano wa kuongezeka kwa bajeti ijayo ya Kenya kutokana na athari za korona

Waziri Yatani aelezea uwezekano wa kuongezeka kwa bajeti ijayo ya Kenya kutokana na athari za korona

Bajeti ya Kenya katika mwaka wa kifedha  2020/2021 inatarajiwa kuongezeka kutokana na athari za virusi vya korona, amesema Waziri wa Fedha, Ukur Yatani.

Yatani ambaye alisema bajeti ya mwaka huu wa kifedha ingepungua kwa asilimia 7.5  ya ukuaji wa pato jumla la taifa, GDP aliposoma bajeti mwezi Juni mwaka huu, amesema bajeti ya mwaka huu itaongezeka kutokana na janga la korona.

Hata hivyo, Waziri Yatani amesema hazina ya kitaifa halina fedha za kutosha hasa ikizingatiwa Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi, KRA ilikosa kuafikia malengo yake baada ya jumla ya mapato kupungua kwa shilingi bilioni arubaini miezi mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa Yatani, serikali inafanya mazungumzo na Benki ya Dunia ili kuipiga jeki bajeti yake hadi mwaka wa kifedha 2021/2022.

 

Iwapo Benki ya Dunia itatoa fedha, huu utakuwa mkopo wa tatu kutoka kwa benki hiyo.