×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto awaonya wanasiasa dhidi ya kuwachochea Wakenya

Ruto awaonya wanasiasa dhidi ya kuwachochea Wakenya

Naibu wa Rais William Ruto amewashauri wanasiasa kukoma kuwachochea Wakenya kwa lengo la kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Ruto amesema kwamba kuna baadhi ya wanasiasa ambao wanaendelea kuwachochea Wakenya huku wakiendeleza ajenda zao za kibinafsi.

Naibu wa Rais amesema kwamba Wakenya kamwe hawatakubali kuwaganywa katika misingi ya vyama na kisiasa ili kuzua ghasia.

Ruto amezungumza katika boma lake mtaani Karen jijini Nairobi wakati wa mkutano wa maombi ambao umehudhuriwa na viongozi wa kisiasa na kidini wa Kaunti ya Narok.

<AUDIO>

Waliohudhuria shughuli hiyo ni Wabunge Lemanken Aramat, Gabriel Tongoyo, Soipan Tuya, Aisha Jumwa, Ndindi Nyoro ,  Kimani Ngunjiri,  Maseneta David Ole Sankok , Mary Seneta,  Gladys Shollei , Steve Lelegwe na  Susan Kihika.

Ruto amesema wanaoendeleza cheche hizo watashangaa kwani Wakenya wako macho kuona ni kiongozi yupi anajali maslahi yao kwa sasa.

Kwa upande wao Nyoro, Kihika na Lelegwe wameendeleza shutma dhidi ya Kinara wa ODM Raila Odinga wakimsuta kwa kupinga michango ya Ruto makanisani.

<AUDIO>

Naye Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amelaani vikali kukamatwa kwa wanasiasa wanaohusishwa na matamshi ya chuki akisema kuwa kumefanywa kimapendeleo. Jumwa amesema kunao wanasiasa ambao wametoa matamshi makali ya chuki na wale hawajawajibishwa.