×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 96 wathibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini Kenya

Watu wengine 96 wathibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini Kenya

Watu wengine 96 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona humu nchini na kufikisha idadi jumla ya maambukizi kuwa elfu thelathini na sita, mia tatu na moja. Watu hao wamethibitishwa kuambukozwa baada ya kupimwa kwa sampuli elfu tatu, mia mbili sabini. Miongoni mwa walioambulziwa, tisini na wawili ni Wakenya huku wanne wakiwa raia wa kigeni. Watu sabini walioambukizwa ni wanaume huku wanawake wakiwa ishirini na sita.

Mtu mchanga zaidi aliyeambukizwa ana umri wa miaka mitano huku mzee zaidi akiwa na umri wa miaka themanini na mmoja. Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa visa 26 huku Kaunti ya Kisii ikiwa ya pili kwa idadi ya maambukizi mapya  yaliyothibitishwa.

Aidha watu wengine 121 wamepona baada ya kuambukiziwa virusi vya korona na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa elfu ishirini na tatu, mia tatu sitini na wanne . Miongoni mwa watu hao 97 walikuwa wakihudumiwa nyumbani huku 24 wakiwa wale waliokuwa hospitalini. Hata hivyo watu wengine 10 wamefariki dunia na kufikisha mia sita thelathini na wanne idadi jumla ya waliofariki dunia.  Francis Kuria ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya ya Umma

Wizara ya Afya imesisitiza kwamba bado maambukizi ya virusi vya korona hayajapungua nchini licha ya idadi ndogo ya visa vipya ambayo imekuwa ikiripotiwa katika siku za hivi karibuni. Daktari Kuria amesema idadi hiyo ndogo imekuwa ikichangiwa na upimaji wa sampuli chache japo wizara inatarajaia kwamba wiki ijayo itapata visaa zaidi vya kuwapima watu.