×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mbunge Alice Wahome apinga kuidhinishwa kwa Mohammed Badi kuhudhuria vikao vya mawaziri

Mbunge Alice Wahome apinga kuidhinishwa kwa Mohammed Badi kuhudhuria vikao vya mawaziri

Mbunge wa Kandara Alice Wahome ameishtaki serikali kufuatia tukio ambapo mkuu wa kitengo cha Nairobi Metropolitan Services Meja Mohammed Badi alihudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Katika kesi hiyo, Wahome amesema kwamba kualikwa kwa Badi kwa kikao hicho ilikuwa ukiukaji mkubwa wa katiba na hivyo kuitaka mahakama kumzuia kiongozi huyo kutohudhuria vikao vingine vya baraza hilo.

Wahome ametetea msimamo wake akisema kwamba serikali ilikiuka katiba kwa kumwalika afisa wa jeshi kwenye kikao cha baraza hilo.

Ikumbukwe kuwa Badi alikubaliwa kuhudhuria vikao hivyo baada ya kuishwa kiapo cha siri wiki iliyopita katika Ikulu ya Nairobi.