×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Gavana Korane na washukiwa wengine wanne wa ufisadi wakana mashtaka ya ufisadi dhidi yao

Gavana Korane na washukiwa wengine wanne wa ufisadi wakana mashtaka ya ufisadi dhidi yao

Gavana wa Garissa, Ali Korane ameshtakiwa rasmi kwa makosa ya ufisadi katika Mahakama ya Milimani muda mfupi uliopita.

Hata hivyo, kiongozi huyo amekanusha mashtaka yote aliyosomewa yakiwemo; kushirikiana na wengine kuiba fedha za umma, uhalifu wa kiuchumi, na utumizi mbaya wa mamlaka.

 

Korane ameshtakiwa pamoja na Ofisa Mkuu wa Idara ya Fedha Ibrahim Malow, Mkuu wa Hazina ya Kaunti hiyo Mohammed Abdulahi, mwenzake Abdi Shale na mkuu wa Idara ya Uhasibu Ahmed Aden.

Gavana Korane amewachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tatu. 

Hakimu Douglas Ogoti ametoa uamuzi huo na kuagiza kwamba Korane asiruhusiwe kuingia ofisini mwake hadi pale kesi ya ufisadi inayomkabili itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Korane amewachiliwa baada ya kukanusha mashtaka ya wizi wa shilingi milioni 233, fedha zilizotolewa kwa ufadhili wa ujenzi wa soko mjini Garissa pamoja na ukarabati mjini humo na Benki ya Dunia.