×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ugali wasababisha mauti kwenye Kaunti ya Kakamega

Ugali wasababisha mauti kwenye Kaunti ya Kakamega

Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Emukaya kata ya Butsotso magharibi eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega baada  ya mwanaume wa miaka 54 kumuua mkewe wa miaka 44 kwa kumpiga kwa jembe wakizozania chakula, akidai kunyimwa ugali.

Kulingana na Sharon Margarita, mwanawe mwendazake amesema alikuwa akilala wakati wa usiku kabla ya kusikia mamake mzazi Florence Nakonjio akipiga mayowe kuwa mmewe Joseph Boyi ambaye wakati huo alikuwa mlevi alikuwa akimpiga kwa jembe.

Ni kisa ambacho kimewakera majirani wakisema ni sharti mhusika atoe kafara ya ng'ombe atakayechinjwa kufanya tambiko ili kuondoa mikasa zaidi

Kwa mujibu wa Naibu Chifu wa sehemu hiyo Titus Muganda, mshukiwa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kakamega, maiti ya mwendazake ikihifadhiwa katika hifadhi ya wafu ya hospitali ya Kakamega.