×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sudi kusalia korokoroni hadi Jumatano wiki hii

Sudi kusalia korokoroni hadi Jumatano wiki hii

Mbunge wa Kapsaret, Oscar Sudi atalazimika kusalia korokoroni hadi Jumatano wiki hii atakapobaini iwapo ataachiliwa kwa dhamana au la.

Sudi amefikishwa katika Mahakama ya Nakuru mbele ya Hakimu Mkuu, Josephat Kalo ambapo Upande wa Mashtaka uliomba azuiliwe kwa siku kumi na nne zaidi kuruhusu uchunguzi kukamilika.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, ODPP kupitia mwendesha mashtaka James Akello imedai kwamba Sudi hapaswi kuachiliwa hasa ikizingatiwa ana ushawishi mkubwa vilevile kuwatishia mashahidi.

Sudi amefunguliwa mashtaka matano yakiwemo; kutoa matamshi ya uchochezi, kumpiga afisa wa polisi, kukiuka maadili, kukataa kukamatwa vilevile kumiliki silaha kinyume na sheria. 

 Hata hivyo mawakili wake Gladys Boss Shollei, Seneta Kipchumba Murkomen na Isaac Terer wamepinga ombi hilo wakisema mteja wao anapaswa kuachiliwa kwa dhamana hasa ikizingatiwa alijiwasilisha katika Kituo cha Polisi cha Kapsaret mapema jana.

Kwa upande wake Seneta wa Nakuru, Susan Kihika, ameendelea kuwaomba wakazi wa Bonde la Ufa kuwa watulivu. Vilevile ameishtumu upande wa mashtaka kwa madai ya kumwongezea mashtaka mbunge huyo.

Sudi amekesha katika KItuo cha Polisi cha Central mjini Nakuru baada ya kujiwasilisha katika Kituo cha Kapsaret kwenye Kaunti ya Uasin Gishu. Baadaye Sudi alisafirishwa hadi Nakuru akiandamana na mawakili wake.